Na Mazengo Jr (Agriculture forum)
Hydroponics ni utaratibu wa kuotesha mimea kwa kutumia maji bila kuhusisha mchanga/udongo kabisa. Mimea inaoteshwa katika chombo maalum "tray" ambacho kipo safi na kina matundu kwa chini ili kusaidia maji yasituame wakati unamwagilia mimea yako.
Tuangalie mfano wa uoteshaji mbegu za ngano kwa njia hii ili zitumike kama chakula cha mifugo kama kuku, ng'ombe, nguruwe, sungura.n.k.

VIFAA:
1.Tray ya plastic au aluminium yenye matundu (umbo lolote tu).
2. Chupa ya kunyunyizia maji (sprayer).
3. Mbegu za ngano au shayiri(chagua ambazo hazijambunguliwa).
4. Chombo cha kulowekea mbegu (ndoo au beseni itafaa).
5. Chujio la plastiki au unaweza tumia kitambaa.
JINSI YA KUANDAA:
1. Pima uzito wa mbegu zako kisha zisafishe kuondoa takataka zote..
2. Weka maji kwenye ndoo au beseni kisha weka mbegu zako ili kuziloweka kwa masaa 4 mpaka 12(unavyoloweka muda mrefu ndio zinaota haraka zaidi).
3. Baada ya kuloweka toa mbegu zako kisha chuja maji kwa chujio au kitambaa safi.
4. Baada ya kuchuja mbegu zako zihamishie kwenye tray kisha zisambaze ili zisibanane sana. (Kama huna trei tumia hata ungo).

5. Baada ya kusambaza mbegu zako kwenye tray funika mbegu zako kwa kitu chochote kama nguo, gunia, kiroba tupu au ungo mkubwa juu yake kwa masaa 48(siku 2). Katika hizo siku mbili kagua mbegu zako kama ni kavu kisha mwagilia maji kiasi kuzilowesha. Hakikisha kifaa unachofunikia kina uwezo wa kupitisha hewa au kina matundu. Endelea kufunika baada ya kunyunyiza maji
6. Baada ya saa 48 mbegu zako zitaanza kuchipua, utaona nyuzi nyuzi nyeupe zimeanza kutoka. Hamishia tray za mbegu kwenye kichanja au eneo lolote lenye hewa ya kutosha lakini zikinge dhidi ya jua kali kwa kuweka turubai au nailoni juu ya kichanja au tumia hata mifuko ya viroba kutengenezea kichanja/kibanda chako. Unaweza pia kutumia neti za mbu kuzungushia kichanja chako ili kuzuia wadudu na ndege kushambulia mbegu zako.
UMWAGILIAJI.
Mwagilia angalau mara 3 kwa siku yaani asubuhi. Mchana na jioni. Hakuna haja ya kumwagilia usiku kwasababu usiku hua kuna unyevu mwingi tu hivyo usishangae hata asubuhi kukuta mbegu zako zina umande.

UVUNAJI.
Unaweza kuvuna fodder zako baada ya siku 4 mpaka 9. Kumbuka kwamba unapoziweka fodder zako muda mrefu zaidi (siku 7 - 9) ndio unapata fodder nyingi zaidi. Lengo ni kupunguza gharama za chakula cha mifugo yako hivyo zalisha kwa wingi. Mfano kilo 2 za ngano huzalisha kilo 4 za fodder ndani ya siku 4 lakini ukiziacha ndani ya siku 7 - 9 zinazalisha kilo 12 - 16 za fodder.
Unaweza kuharakisha uvunaji wako wa fodder kwa kupiga foliar fertilizer (booster au D.I).

UPATIKANAJI WA CHAKULA MUDA WOTE.
Ili uweze kuhakikisha chakula cha njia hii kinakua tayari muda wote kwa malisho ya mifugo yako ni lazima ujue mahitaji halisi ya chakula kwa siku. Kwa mfano kama kuku wako wanakula kilo 25 za chakula kila siku, na kilo 2 za ngano zimekupatia kilo 16 za fodder ndani ya siku 8, basi utahitaji kiasi gani cha mbegu kuzalisha kila siku? Chukua kilo 25 za chakula gawanya kwa kilo 16 za fodder ulizopata kutoka kilo 2 za mbegu. Utapata 1.5625 na jibu hili zidisha kwa 2 (kiasi cha mbegu kilichozalisha kilo 16 za fodder). Jibu lake itakua kilo 3.125 za mbegu utazohitaji kuotesha kila siku ili kuweza kuwalisha kuku wako.
Zoezi hili ili kua endelevu utahitaji kua na tray walau 8 ili kila siku upande tray 1. Hakikisha tray inatosha kutandaza mbegu zako na kama haitoshi basi utalazimika kua na tray ndogo ndogo nyingi ili kutosha hizo kilo 3.125 za mbegu kila siku.

USHAURI.
Ili kuku wako wasipate dhida ya mmeng'enyo wa chakula basi wape pumba kavu au punje za mahindi kidogo kila baada ya siku 1 au 2. Virutubisho vilivyomo kwenye fodder vinatosha kabisa kukuza mifugo yako bila shida yoyote.
Fodder za shairi hukua haraka zaidi kuliko ngano. Kama unaweza kuzipata ni bora zaidi kuliko ngano. Kwa wale ambao hatuwezi kupata mbegu za ngano au shayiri basi unaweza kutumia mbegu hata za mtama.
Kwa wale ambao tunaweza kulima ngano au shayiri basi tufanye hivyo kwa faida ya mifugo yetu.

MAHITAJI YA KUKU KWA SIKU.
kwa kawaida kuku mmoja mkubwa hula gramu 125 mpaka 150 za chakula kila siku. Kama una kuku 500 basi utahitaji 500*135 gram za chakula kila siku. Kilo 67.5 za chakula cha kawaida tukizibadili kuwa fodder utahitaji 67.5/16*2 za mbegu za fodder kila siku. Utapata kilo 8.4 za mbegu.
Gharama. Kilo moja ya chakula ni 700(mfano). Gharama za chakuka cha kawaida itakua 67.5*700 utapata jumla ni 47,250/. Gharama za mbegu ni kilo 8.4 kilo 1 ya mbegu ni 2,000. Gharama ni 2000*8.4. Sawa na 16,875/. Kwa siku utaokoa kiasi cha 47,250 - 16,825. Utapata 30,425.
Makosa madogo madogo yanayofanyika wakati wa utowaji chanjo kwenye Kuku na hatimaye chanjo kutofanya kazi vizuri.
1.maji yakuchanganyia.
Unaponunua chanjo yoyote ile yenye Maelezo yakuchanganya na maji basi hakikisha unatumia maji ya kisimani au ya vua na si maji ya bombani kwasababu maji hayo yanachrolini ambayo inafanya kanzi yakuuwa wadudu kwavile chanjo yako ni wadudu unapochanganya maji ya bomba hakuna ubishi hapo kama unaiuwa hiyo chanjo nakujikuta unawapa maji yakawaida.
Na kama utakosa kabisa maji ya kisimani au maji ya vua basi anaweza kuchukua maji ya bomba na kuyachemsha mbaka yachemke then unaacha ya poe kabisa kisha unachanganya na chanjo yako.
Kwanini uchemshe? (Jibu: ilikuuwa ile cl isifanye kazi.)
2.Hakikisha Kuku wako cku mbili zilizo pita hujawapa antibiotic antibiotic yoyote ile kwani kazi ya antibiotic nikuuwa wadudu sasa chunga sana leo umewapa dawa kisha unawapa chanjo ni kosa haita fanya kazi vizuri.
3.maji ya chanjo wape Kuku na wasiyanywe zaidi ya masaa mwili.
4.Hakikisha unachovya vichwa Vya Kuku ndani ya maji yaliyo changanywa na chanjo ili iweze kuingia machoni na puani humo ndimo wadudu wa chanjo huzaliana kabla yakusambaa mwili kwaajili ya kupambana na vimelea Vya magonjwa. Yale maji yanayoenda tumboni hayana Kazi ila yale yanayo gusa pua wakati wa kunywa ndio yanayo fanya kazi kwasbabu kunagrand zinapatikana puani na hizo zinazo patikana puani zinapatikana pia machoni ndo maana nasema unatakiwa kuchovya vichwa ndani ya maji ya chanjo.

No comments:
Post a Comment