Na Mazengo Jr (Agriculture forum)
Hydroponics ni utaratibu wa kuotesha mimea kwa kutumia maji bila kuhusisha mchanga/udongo kabisa. Mimea inaoteshwa katika chombo maalum "tray" ambacho kipo safi na kina matundu kwa chini ili kusaidia maji yasituame wakati unamwagilia mimea yako.
Tuangalie mfano wa uoteshaji mbegu za ngano kwa njia hii ili zitumike kama chakula cha mifugo kama kuku, ng'ombe, nguruwe, sungura.n.k.

VIFAA:
1.Tray ya plastic au aluminium yenye matundu (umbo lolote tu).
2. Chupa ya kunyunyizia maji (sprayer).
3. Mbegu za ngano au shayiri(chagua ambazo hazijambunguliwa).
4. Chombo cha kulowekea mbegu (ndoo au beseni itafaa).
5. Chujio la plastiki au unaweza tumia kitambaa.
JINSI YA KUANDAA:
1. Pima uzito wa mbegu zako kisha zisafishe kuondoa takataka zote..
2. Weka maji kwenye ndoo au beseni kisha weka mbegu zako ili kuziloweka kwa masaa 4 mpaka 12(unavyoloweka muda mrefu ndio zinaota haraka zaidi).
3. Baada ya kuloweka toa mbegu zako kisha chuja maji kwa chujio au kitambaa safi.
4. Baada ya kuchuja mbegu zako zihamishie kwenye tray kisha zisambaze ili zisibanane sana. (Kama huna trei tumia hata ungo).