Saturday, 30 April 2016

Ufugaji wa NYuki

Na Pretty Development for Poverty Reduction (PDPR) 0754397178, 0652556833, Njombe.

Ufugaji wa Nyuki ni miongoni mwa fursa za ujasiriamli zilizosahaulika
nchini Tanzania kutokana na uelewa mdogo wa jamii na ukosefu wa
taarifa sahihi za mradi licha ya kuwa faida nyingi kutokana na uwepo
wa mazao mengi ya Nyuki kama Asali, Nta, gundi (Mpuya), pollen, na
kuwa mawakala wa uchavushaji wa mazao.
Mradi wa ufugaji nyuki unahitaji mtaji Mdogo, eneo dogo, muda mchache
wa kusimamia na unavihatarishi vichache (Risk) na unafaida kubwa kwa
kipindi kifupi,
Kwa mfano Asasi ya PDPR inauza mzinga mmoja wa aina ya ubao wa juu kwa
TSH: 45,000/= ambao unauwezo wa kutoa lita 25 hadi 30 kila baada ya
miezi 5 na kwa mwaka unaweza kulina mara mbili,
Mzinga mmoja unauwezo wa kukuzalishia kiasi cha TSH: 250,000/= hadi
400,000/= kwa mwaka kama mfugaji utafuata kanuni za ufugaji bora wa
Nyuki kama kwa kujenga Nyumba ya Nyuki (bee house), kuweka vijengeo
vya kuwalishia Nyuki, kupanda mimea inayo wavutia Nyuki kama Mirejea,
alizeti na mbaazi.

Ufugaji wa nyuki wa kutumia Bee house unasaidia kupunguza eneo la
kufugia, Nyumba ya mita 9 kwa 3 inachukua mizinga 50.
GHARAMA ZA UWEKEZAJI KWA MIZINGA 20
Ununuzi wa mizinga 10 …        900,0000
Ujenzi wa nyumba ya nyuki     200,000
Utundikaji wa mizinga              30,0000
Ununuzi na upakaji wa Nta     10,0000
Gharama zinginezo                    50,000
JUMLA                                      1,190,000/=
Mapato ya Mizinga 20
Mzinga mmoja unatoa wastani wa lita 25 hadi 30 za Asali kwa msimu
mmoja wa miezi 5 na kwa mwaka unaweza lina mara mbili au tatu
inategemeana na jinsi unavyo wahudumia na hali ya hewa ya eneo husika.
Kwa makadilio tunaweka unaweza pata asali lita 20 kwa kila mzinga kama
under estimation.
Mizinga 20 X lita 20 sawa na lita 400 Za Asali ambapo kila lita huuzwa
kati ya TSH: 10,000 hadi 15,000 ina maana mradi wako unauwezo wa
kuzalisha milioni 4 hadi 6 kwa mwaka kwa makadilio ya chini ya asali
ambapo bado hatujaangalia Nta ambayo tunaweza kupata KG 2 kwa kila
mzinga na jumla KG 40 ambapo kilo moja huuzwa TSH: 15,000 hadi 40,000
ikitegemea na mnunuzi ambapo utaweza kupata mapato ya laki sita na
ukiwa hujauza Mpuya.
Asasi ya Pretty Development for Poverty Reduction (PDPR) inauza
mizinga ya ubao wa juu kwa TSh: 45,000 na commercial bee hive kwa Tsh:
110,000 na kwa wafugaji wadogo inawashauri watumia mzinga wa ubao wa
juu kwa kuanzia.
Na kila mteja anayenunua mizinga zaidi ya 25 anajengewaNyumba ya Nyuki
bure na kuwekewa mizinga na kila mteja anayenunua mizinga kwetu
anapewa kitabu cha ufugaji nyuki, mafunzo na ushauri wa mwaka mmoja
bure. Na soko la Mazao ya Nyuki lipo la Uhakika.
Kwa maelezo zaidi piga simu 0754397178, 0652556833 au tembelea
www.envaya.org/pdpr kwa maelezo zaidi. pia tunauza chakula cha kuku,
vifaranga, mashamba ya miti ya mbao, egg incubator, na tuna vitabu vya
ufugaji kuku, Tupo Njombe na offisi ndogo ipo Ubungo kibo Dar es
salaam.

No comments:

Post a Comment